Monday, 26 January 2015

...Nimecheka sana, hebu cheka na wewe..

...Nimecheka sana, hebu cheka na wewe..Mtanzania, Mkenya na Mganda walikamatwa China kwa kukosa vibalì, wakaambiwa wachague adhabu ya kifo au kwenda porini kuleta matunda kumi ya aina moja kila mmoja;
Mganda akaleta machungwa akaambiwa ameze moja moja hadi yaishe bila kufumba macho, kucheka, wala kulia; akameza moja akaanza kulia, akapigwa risasi akafa.
Baada ya muda Mkenya akaja na zabibu akameza alipofika ya tisa akacheka, akauawa.
Walipofika kuzimu Mganda akamuuliza Mkenya, ulishindwa nini wakati matunda yako madogo? Mkenya akajibu, "Nilicheka kwa sababu Mtanzania alikuwa njiani anakuja na matikiti.

No comments:

Post a Comment