Wednesday, 11 February 2015

Visa vya kupiga deki

Askari wameitwa kwenye nyumba ambayo kuna ugomvi. Wakafika alafu ikabidi waripoti kwa simu yale waloyakuta
Askari: mkuu tumekuja hapa tumekuta mama wa nyumba amempiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza sana
Afande: kisa na mkasa gani hata akafanya hivyo
Askari: mama alikua anasafisha jikoni na kupiga deki, sasa mumewe akaingia jikoni na viatu kabla sakafu haijakauka
Afande: mushamkamata huyo mama??
Askari: hapana bado mkuu
Afande: mnangoja nini sasa??
Askari: tunangoja sakafu ikauke afande

No comments:

Post a Comment