Friday, 30 January 2015

Mtoto ana akili huyo

Mtoto: Mwalimu mimi nataka
nisome darasa la
nne kwani hili la3 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema
hivo?
Mtoto: Nina akili...
Basi mwalimu kamueleza mkuu
wa shule na
mkuu kaitisha interview kwa
dogo.
Maswali ni haya....
Mwalimu: Kwenye ndege kuna
matofali 20
tukitoa moja tukalidondosha
chini yatabaki
mangapi?
Dogo: Yatabaki 19.
Mwalimu: Nipe hatua za
kumuweka tembo
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamuweka
tembo kisha
unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za
kumuweka nyani
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa
tembo
ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga
friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku
ya kuzaliwa
kwa simba, wanyama wote
wameenda kasoro
mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu
tumemuweka
kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka
mto unaokuwaga
na mamba na viboko wakali,
aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na
viboko nao
walienda kwenye sherehe ya
kuzaliwa kwa
simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee
alivuka mto,
baadae alikufa. Unadhani kwa
nini?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali
tulotoa
kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu: Huyu dogo
akasome chuo
kikuu ....����✋

No comments:

Post a Comment